AHAZI

AHAZI

Friday, March 15, 2013

Masanja Mkandamizaji

Jamaa fulani alikuwa anataka kuoa. Sasa siku ya mazoezi ya ndoa akamfuata mchungaji popompo akamwambia: mchungaji, laki 2 hii hapa, siku ya ndoa ikifika ile sehemu ya kusema "Je, unaahidi kukaa naye kwa shida na raha hadi kifo kiwatenganishe?" wewe iruke hiyo sehemu. Mchungaji akakubali. Basi siku ya ndoa ikafika. Ilipofikia ile sehemu mchungaji akasema; "Je, unaahidi kukaa naye kwa shida na raha na karaha zote na kumtumikia mkeo kama mtumwa na kumpenda na popote utakapopita ukikutana na wanawake wengine uwe unakimbia na kuwahi nyumbani na kuicha vikao vya mipira na mambo mengine hadi kifo kiwatenganishe?" Jamaa akakasirika, kabla ya kujibu akamnong'oneza mchungaji: Hivi mimi na wewe tulikubaliana nini? Mchungaji akaingiza mkono mfukoni akatoa laki 2 akampa jamaa halafu akamwambia: Samahani ila binti huyu alikuja akatoa laki 5.

No comments:

Post a Comment