AHAZI

AHAZI

Friday, March 15, 2013

prof and mbeba mizigo

Profesa mmoja wa chuo kikuu na rafiki yake mbeba mizigo waliamua kwenda mbali kutembea lakini hakukuwa na nyumba kwa hiyo wakalala ndani ya hema. Katikati ya usiku yule mbeba mizigo akamuasha rafiki yake profesa akamwambia: Angalia juu unaona nini na unatambua nini? Profesa akajibu: naona nyota na mwezi na natambua kwamba nyota ziko mbali zaidi na sayari yetu ya dunia ndo maana zinaonekana ndogo. Pia mwezi, jifunze kwamba mwezi huakisi mwanga wa jua na kuna sayari ambazo hazina mwezi. Lakini pia mambo kama haya ni mazito kuelewa na mbulula kama wewe ni ngumu zaidi ku-understand. Profesa alipomaliza akamuuliza mbeba mizigo: wewe unaona nini na unatambua nini? Mbeba mizigo akajibu: mimi naona nyota na anga na natambua kwamba hapa tulipo hema letu tayari limeibiwa na tumelazwa nje ya hema na ni porini, maana tulivyoingia ndani ya hema tulikuwa hatulioni anga, na hizo sauti za wanyama kwa mbali zinanitambulisha kwamba hatuko salama na inabidi tuanze kutafuta sehemu ya kujisitiri na jambo kama hili ni vigumu kwa wewe mbulula+ kuelewa.

No comments:

Post a Comment