AHAZI

AHAZI

Saturday, March 2, 2013

du

Jamaa kakamatwa kwa kosa la wizi wa mamilioni ya vijisenti akahukumiwa kwenda jela akafungwa. Baada ya miezi miwili baba yake akamuandikia barua kwenda gerezani, jamaa akaipokea: "Mpendwa mwanangu, hali yangu ya uzee unaijua, moyo unaniuma na natamani ungekuwa hapa msimu huu wa kupanda unisaidie kulima lile shamba kule bondeni kwa ajili ya kupanda viazi, lakini sina jinsi, nafsi itaendelea kuuma na nitakusubiri mpaka mwaka utakapoaachiwa huru." Gerezani kawaida barua huwa zinasomwa kwanza na polisi magereza. Siku iliyofuata jamaa akaandika barua kumjibu baba yake: "Baba tafadhali sana wala usijaribu kulima hilo shamba la kule bondeni, pale ndipo nilipoyahifadhi- yale mamilioni niliyoiba, tutaonana Mungu akipenda." Siku iliyofuata mzee akashtukia askari kibao wamevamia shamba na kulilima kila kona lakini hawakupata kitu. Baadaye jamaa akamuandikia baba yake barua tena: "Mpendwa baba, huo ndo ulikuwa msaada ambao ningeweza kufanya, unaweza kupanda viazi sasa, kwaheri."

1 comment: