AHAZI

AHAZI

Sunday, July 3, 2016

Maharagwe ya nazi



MAHARAGE YA NAZI

Maharage kikombe kidogo 1 ya kawaida au yanaozwa kwenye kikopo
Nyanya ya kopo nusu au robo kikombe (Tomato sause/purée)
Chumvi kiasi
Thomu kijiko cha chai 1
Tangawizi  kijiko cha chai 1
Nazi ya kopo kibati kimoja au unaweza ukakuna nazi ukawa na tui zito
Pilipili boga kiasi
Kitunguu maji kiasi
Mafuta ya kupikia kiasi

**Chemsha maharage yako yakishaiva yamwage maji au Kama maharage ya kopo mwaga maji na uweke pembeni**
**Weka mafuta ya kupikia kwenye sufuria lako na ukaange kitunguu maji, pilipili boga, tangawizi na thomu***
**Vikishaiva weka nyanya yako ya kopo ikaange kidogo Kisha weka maharage**
**Yaache maharage Kama dakika mbili, Kisha weka nazi yako na usisahau kuweka Chumvi**
**Epua maharage yako nazi ikiiva, usiache yakauke sana**



aPosted via Blogaway

No comments:

Post a Comment