*BUSTANI YA MFUKO/GUNIA*
*Mahitaji*
1. Chukua mfuko, gunia au salfate,
2. Andaa udongo, mchanga na mbolea kwa ratio ya 1:1:1
3. Andaa kokoto.
4. Kopo kisadolin hawa kikiwa kile chenye mfumo wa pipa ili kiwe na kipenyo sawa pande zote then litoboe hilo kopo liwe waz pande zote
*Utengeneza*
*i* Changanya mchanganyiko wa udongo, mbolea na mchanga
*ii* chukua mfuko wako ufunue uwe wazi ikibid uukunje ili kimo kipungue kidogo
*iii* weka kopo lako ktkt ya mfuko lijaze kokoto hilo kipo
*iv* weka udongo wako uliouandaa kwenye mfuko had kufikia kimo cha kopo lako.
*v* livute juu hilo kopo ili kokoto zibak livute had lifikie usawa wa juu zilipoishia kokoto zako za kwanza
*rudia kuweka kokoto, na udongo kama (iii) na (iv) alafu then namba (v) had ufikie juu usawa wa mfuko wako.*
VI. Toboa mfuko kwa umbal wa cm15 kati ya shimo na na shimo kama unapanda chines, sukumawik na mimea inayofanana na hiyo.
*bustan ya mfuko inafaa kupanda mboga mboga na ni rahisi kuhudumia*
*Note* unapoweka udongo hakikisha unashindilie ili utakapomwagia maji mfuko usijikunje
*unapomwagilia maji mimina kwenye kokoto na udongo wote utapata maji*
aPosted via Blogaway
No comments:
Post a Comment