*SOMA HII NA CHEKA KWA KUONGEZA AFYA.*
*Mwelevu na Mjinga walienda ktk usaili, walipofika kabla hawajaingia wakakubaliana aanze Mwerevu kisha akitoka ampe majibu Mjinga ili wote wapate kazi.*
*Basi Mwerevu akaingia na maswali yakawa hivi:-*
*Msaili:- Tanzania ilipata Uhuru mwaka gani?*
*Mwerevu:- ilitakiwa iwe mwaka 1960 ila ikasogezwa mpaka 1961 kutokana na sababu mbalimbali..*
*Msaili:- Nani hasa alihusika na upatikanaji wa Uhuru huo?*
*Mwerevu:- Kuna watu wengi walihusika ila Mwl. J.K. Nyerere ndiye alikuja kumalizia.*
*Msaili:- Inasemekana katika sayari ya Mars kuna viumbe wanaishi, je ni Kweli?*
*Mwerevu:- Watu wengi wanasema hivyo lakini haijathibitishwa na wanasayansi.*
*Baada ya Mwerevu kutoka basi Mjinga akapewa majibu yote..*
*Kuingia ktk usaili maswali yakawa hivi:-*
*Msaili:- Tuambie ulizaliwa mwaka gani?*
*Mjinga:- Ilitakiwa iwe mwaka 1960 ila ikasogezwa mbele mpaka mwaka 1961 kutokana na sababu mbali mbali.*
*Msaili:- Mungu Wangu, BABA yako anaitwa nani?*
*Mjinga:- Kuna watu wengi walihusika ila Mwl. J. K. Nyerere ndiye alikuja kumalizia .*
*Msaili:- Hivi wewe ni chizi?*
*Mjinga:- watu wengi husema hivyo lakini haijathibitishwa na wanasayansi*😂😂😂
aPosted via Blogaway
No comments:
Post a Comment