AHAZI

AHAZI

Thursday, April 14, 2016

Cheka kidogo

Jamaa Mmoja Alikuwa Safarini Gari
Likamharibikia Kijijini Akaomba Hifadhi
Akakaribishwa Baada Ya Kuoga Na Kula.
Mzee: Sasa Sijui Huyu Mgeni Atalala Wapi?
Mke: Sa Hizi Ni Usiku Akalale Na Bebi.
Jamaa Akaona Huyu Bebi Pengine Ni Mtoto
Anakojoa Kitandani Au Akalia Asije
Akamsumbua Usiku.
Jamaa: Msipate Tabu Mi Nitalala Hapa Kwenye
Kochi.
Akalala, Asubuhi Wakawa Wanakunywa Chai
Akaibuka Mrembo, Jamaa Akapigwa Mshangao
Nusu Ajimwagie Chai.
Binti: Naitwa Bebi We Unaitwa Nani?
Jamaa Akasema " Mi Naitwa Fala😂😆😆😆😆😆😆😆😆😆



aPosted via Blogaway

Tuesday, April 12, 2016

JKT

TANGAZO

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, anawatangazia vijana wenye sifa za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea kwa mwaka 2016.

Barua zilizoainisha sifa za kijana kujiunga na mafunzo ya JKT zimetumwa kwa Waheshimiwa Wakuu wa mikoa. Mchakato wa zoezi la kuwapata vijana wenye sifa unaanza Aprili 2016 hadi tarehe 20 Mei 2016.

Sifa za mwombaji ni kama zifuatazo:-

1. Awe raia halisi wa Tanzania.

2. Umri. Kwa vijana wenye elimu ya Darasa la saba hadi kidato cha sita ni miaka 18 hadi 23.Vijana wenye elimu ya Stashahada umri ni miaka 18 hadi 26 na Vijana wenye elimu ya Shahada na kuendelea umri ni miaka 18 hadi 30.

3. Awe na afya njema, akili timamu.

4. Asiwe na alama yeyote ya michoro mwilini (Tattoo).

5. Mwenye tabia nzuri, hajapatikana na hatia Mahakamani na hajawahi kufungwa.

6. Kwa vijana waliomaliza elimu ya Sekondari kidato cha nne wawe waliomaliza kuanzia mwaka 2010, 2011, 2012, 2013 na 2014 wenye ufaulu ufuatao:-

      (a) Waliomaliza 2010 hadi 2012 wawe wamefaulu na wawe na alama (Points) zisizopungua 32.

      (b) Waliomaliza 2013 wawe wamefaulu na wawe na alama (Points) zisizopungua 38.

      (c) Waliomaliza 2014 wawe wamefaulu na wawe na GPA isiyopungua 0.6.

7. Awe na elimu ya msingi aliyehitimu darasa la saba.

8. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate).

9. Awe na cheti halisi cha kumaliza shule (School Leaving Certificate)

10. Awe na cheti halisi cha matokeo (Original Academic Certificate/Transcript).

11. Asiwe ametumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au KMKM wala kuajiriwa na Idara nyingine Serikalini.

12. Asiwe amepitia JKT Operesheni za nyuma.

13. Asiwe amejihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, bangi na yanayofanana na hayo..

Waombaji wenye sifa wapeleke maombi yao kwa Waheshimiwa wakuu wa mikoa.

Makao Makuu ya JKT hayatapokea na hayapokei maombi yoyote, kwa vijana watakaoomba nafasi hizo wazingatie maelekezo yatakayotolewa kuepuka usumbufu.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Habari na Uhusiano

Makao Makuu ya JKT

Tarehe 05 Aprili 2016

Source
http://www.jkt.go.tz/component/k2/item/631-taarifa-kwa-umma.html



aPosted via Blogaway

Friday, April 8, 2016

Je unaukumbuka wimbo huu

1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.

2. Akatamka mgonjwa,
ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa,
haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,
kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini,
kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani,
maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani,
sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani,
mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali,
itufae maishani

4. Baba aliye kufani,
akajibu lile swali,
Ninakufa maskini,
baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni,
kama mnataka mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba,
baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba,
hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba,
hazijajua methali,
Kama tunataka mali,
tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni,
nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani,
mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani,
kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja,
fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja,
roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari,
watoto wale wawili,
wakakata na shauri,
baada ya siku mbili,
wote wakawa tayari,
pori nene kukabili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani,
mbegu nyingi mbalimbali,
tangu zile za mibuni,
hadi zitupazo wali,
na mvua ikaja chini,
wakaona na dalili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia,
bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia,
wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe,
majike kwa mafahali,
wakapata na vikombe,
mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe,
sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao,
na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao,
wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao,
wakaandika kauli...

"KAMA MNATAKA MALI
MTAIPATA SHAMBANI".
🚶🚶🚶🚶🚶🚶

Miaka hiyo tuliimba tu kama kujifurahisha wala hatukujua maana yake, leo twatambua nini maana yake, nasisitiza, kama mnataka mali mtaipata shambani



aPosted via Blogaway