*Elimu kutoka tume ya utumishi ya walimu (TSD).*
*WAJIBU MKUU WA MWALIMU TUME YA UTUMISHI WA UMMA
IDARA YA UTUMISHI WA MWALIMU*.
Wajibu mkuu wa mwalimu ambao ndio NGUZO TANO za kazi ya ualimu ni:-
1.KWA MTOTO
2.KWA JUMUIYA
3.KWA KAZI YAKE
4.KWA TAIFA
*1. KWA MTOTO*
Nguzo hii inamtaka mwalimu akubali kwamba wajibu wake mkuu ni kwa mtoto ambaye
amekabidhiwa kumleana kwamba kwa wakati wote anatakiwa kumwongoza kwa kumkuza na kumwendeleza
kimwili, kiakili na kiroho.
*2. KWA JUMUIYA*
nguzo hii inamtaka mwalimu kuijua jumuiya ambamo anaishi
na kufanyia kazi na kutii mamlaka halali na tabia yake mwenyewe kuwa mfano bora kwa wanajumuiya.
*3. KWA MWAJIRI WAKE*
Nguzo hii inamtaka mwalimu kumtumikia mwajiri wake kwa utii na kwa uaminifu kwa mujibu wa masharti ya kazi ya ualimu.
4. KWA KAZI YAKE YA UALIMU
Nguzo hii inamtaka Mwalimu kufuata kwa wakati wote na kwahali ya juu kabisa Maadili mema ya
kazi ya ualimupamoja na:-
- kufanya kazi kwa bidii na kwa kufuata utaratibu
-Kuwa mfano mzuri katika tabia wakati wote
kwa watoto waliochini ya ulinzi wake na hata
watoto wengine katika jamii.
-kujaribu kila wakati kuinua kiwango cha
utendaji nauwezo wa kufanya kazi
-kutotumia vibaya haki zinazoambatana na
utumishi wa umma.
*5. KWA TAIFA LAKE*
Nguzo hii inamtaka mwalimu kuwa mzalendo na raia mwema na mtii wa sheria za nchi na
mwelekezaji wa watoto kuwa wazalendo safi na raia wema
wa baadae kwa kuzingatia wajibu wa mwalimu kwa kazi yake ya ualimu.
Mwalimu anategemewa kuwa na tabia na mwenendo mzuri wa kufaa kuigwa na kustahili kupewa heshima na kuaminiwa na jumuia,wazazina wanafunzi.
Mwalimu yeyote anayekwenda kinyume na maadili na masharti ya kazi ya ualimu anakuwa nimtovu wa nidhamu.
* HAKI ZA MWALIMU*
*LIKIZO YA MWAKA (Annual leave).*
Kwa mujibu wa kanuni za kudumu za watumishi wa umma 2009 kifungu H.5 (ii) kikisomwa pamoja na kanuni za utumishi wa umma, 2003 kifungu cha 97(i) mtumishi wa umma anayostahili yeye kupewa likizo siku 28 kila mwaka.Aidha kifungu cha 97(ii) kinaeleza kuwa likizo ni haki ya mtumishi.
Inapokuwa haitolewi na mwajiri kwasababu mbalimbali basi mwajiri atawajibika kumlipa
mtumishi mshahara wake wa mwezi.Mtumishi hatopewa
likizo ya mwaka hadi amefikisha miezi 8 tangu kuajiliwa rasmi (kanuni Na.97:za 2003). Mtumishi
atapewa usafiri wa likizo mara moja ndani ya mzunguko wa miaka miwili yeye, mkewe na
watoto wane chini ya umri wa miaka 18 au wategemezi, kanuni Na.97(5).
*LIKIZO YA UZAZI(Maternity leave).*
Kifungu Na.98(1),2003 Mtumishi wa kike atapewa likizo ya uzazi siku 84 mara moja kila baada ya
miaka (3) kumaliza likizo yake,akijifungua mapacha atastahili likizo ya siku 100,kwa kwa mujibu wa T.S.S,2008,47(1) Kifungu 98 (2 ) Mtumishi anapojifungua kwa bahati mbaya mtoto akafariki kabla ya miezi 12 kumalizika.
Akipata mimba tena atastahili likizo ya uzazi siku 84 kifungu Na. 98 (3). Mtumishi aliyejifungua atastahili muda wa saa mbili kwenda kunyonyesha hadi kipindi cha miezi sita (6). Mtumishi wa Kiume, mkewe akijifungua atapewa likizo ya siku tatu (T.S.S 48).
*LIKIZO BILA MALIPO.*
Kifungu Na.99 (1) cha kanuni za utumishi wa umma 2003.Katibu Mkuu ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma anaweza
kutoa likizo bila malipo kama ataridhika na sababu za maombi ya likizo hiyo.Hata hivyo maombi hayo ni lazima yapitie kwa Mwajiri kanuni 99(2).
*LIKIZO YA UGONJWA.*
Kifungu Na.100 (1) cha ushauri wa
Daktari,Mamlaka ya ajira inaweza kutoa likizo ya ugonjwa.
Likizo hutolewa miezi sita na mshahara kamili na miezi sita mingine kwa nusu mshahara.
*SABATICAL LEAVE.*
Kifungu 101 (1) Likizo hii hutolewa kwa mwajiri ili kukamilisha au kuimarisha uzoefu.
Likizo hii ni lazima iindhinishwe na Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Likizo hii hupewa Mtumishi si zaidi ya miezi 12 na hutolewa baada ya Mtumishi kufanya kazi
mfululizo miaka mitano,Kanuni Na.101 (4).
*LIKIZO YA KUSTAAFU (Leave Pending retirement)*
Kanuni Na 102 za 2003,Mtumishi wa Umma atastahili kuomba likizo ya kujiandaa kustaafu
mwezi mmoja kabla ya tarehe rasmi ya kustaafu kwake.Atastahili kupewa usafiri wa kumrejesha kwao yeye na familia yake pamoja na mizigo sio chini ya tani tatu kulingana na daraja lake.
*MATIBABU KWA WATUMISHI WA UMMA*
Kifungu .K.(i) za kanuni za kudumu 2009
ikisomwa pamoja na kifungu cha
105 cha kanuni za Utumishi wa umma Mtumishi anastahili kupata matibabu bure.
Hata hivyo kuna utaratibu wa bima ya afya.
Mtumishi akilazimika kusafiri kwenda Hospitali ya Rufaa mwajiri atahusika kugharamia posho ya kujikimu na nauli.
Vitu muhimu.
Barua ya rufaa.
Barua ya ruhusa toka kwa mwajiri
Fomu Appendix K 28$29
Fomu ya madai ya posho.
Fomu Appendex K/V ya madai ya nauli ikiambatana na tiketi K.26.
Kadi ya mahudhurio yahospitali (SICKSHEET).
*FIDIA YA KUUMIA KAZINI.*
Kanuni Na.111(1-5) inaeleza hatua
mbalimbali za kufuata pindi mtumishi anapopatwa na matatizo kazini.
Mtumishi anayeumia atalipwa fidia sio chini ya shilingi 1,000,000/= na sio zaidi ya shilingi 10,000,000 hutegemea na hali ya maumivu au kufariki.
Kifungu cha 110 kinaelezea kwamba mtumishi anapoumia wakati wa kutekeleza majukumu ya ajira yake anastahili fidia na inamtaka mtumishi huyo kujikinga na hali ambayo inaweza kuathiri afya yake.
*KUJIENDELEZA KITAALUMA*
Kanuni Na .103 inaeleza kamba ni wajibu wa mwajiri kuwaendeleza watumishi wake.
Kutokana na tathimini ya kazi , mwajiri atabainisha mahitaji ya
kuendeleza watumishi.
Watumishi ni lazima wajiendeleze katika fani kwa lengo la kuboresha ufanisi.
Kuandaa mpango kazi wa mafunzo kwa watumishi.
-Vitendo vyovote vinavyopingana na utaratibu za kiutumishi
-Uzembe unaomgharimu mwajiri
-kuiuka maadili ya kazi ya ualimu(ya utumishi wa umma).
*ADHABU ZAKE*
-kufukuzwa kazi bila Utumishi.
-kufukuzwa kazi na utumishi.
-kushushwa cheo.
-kushushwa mshahara si chini ya kiwango ulichoanzia kazi.
-kulipa gharama au sehemu ya gharama kwa upotevu au uharibifu uliotokana na uzembe
-karipio
-Onyo
-Kusimamishwa nyongeza ya mshahara.
*KUTOENDELEA NA MAJUKUMU KWA KUPUMZISHWA*
Mtumishi anapumzishwa bila kusimamishwa kazi na bila kuathiri maslahi yake..Lengo lake ni kuzuia kosa lisiendelee kutendeka wakati wa uchunguzi
wa awali ukifanyika,(kanuni Na.37)
*KUSIMAMISHWA KAZI*
Mtumishi husimamishwa kazi na kupewa hati ya mashtaka.Hatua hii ni baada ya Mamlaka ya nidhamu kuridhika kuwa kuna tuhuma za ukweli dhidi ya mtumishi husika.(kanuni 38).
*KUREKEBISHA MASHTAKA*
Mamlaka ya nidhamu inaruhusiwa kurekebisha mashtaka yasiyo sahii ndani ya siku zisizozidi 30 tangu Mshtakiwa alipopewa mashtaka ya awali (kanuni ya 38(3) ).
*NUSU MSHAHARA.*
Mtumishi aliyesimamishwa kazi anastahili nusu mshahara wake wa mwezi tu kwa kipindi chote alichosimamishwa kazi.Iwapo mtumishi husika hatapatikana na hatia na hivyo kutofukuzwa kazi au kutopewa adhabu yoyote atalipwa nusu mshahara wake ambao hakulipwa wakati aliposimamishwa kazi lakini ameadhibiwa kwa adhabu nyingine, atalipwa robo ya mshahara wake. (kanuni ya 38-2,5 na 6).
*KUONDOKA KITUONI MTUMISHI ALIYESIMAMISHWA KAZI.*
Mtumishi aliye simamishwa kazi haruhusiwi kuondoka kituoni bila kuruhusiwa kwa maandishi na mamlaka yake ya nidhamu kanuni ya 38(7).
*ATHARI ZA KUFUKUZWA KAZI*
Mtumishi akifukuzwa kazi hupoteza haki zake.
Hata hivyo mtumishi husika atalipwa pensheni ya mkupuo iwapo wakati huo alistahili pensheni ya kila mwezi.Aidha, mtumishi aliyetiwa hatiani kwa makosa ya jinai yanayohusu rushwa au hujuma,atapoteza haki au madai yake yote. (Kanuni ya 40.2003).
*MTUMISHI ANAPOKABILIWA NA KESI YA JINAI.*
Mtumishi husika atasimamishwa kazi hadi kesi husika itakapohitimishwa.Hatua
za kinidhamu hazitachukuliwa au kuendelezwa dhidi yake.Masharti na maelekezo yote yako kwenye kanuni ya 50 na 51.
*RUFAA*
Mtuhumiwa atapewa haki yake ya kukata rufaa kwenye MAMLAKA SAHIHI na MUDA
MUAFAKA. Rufaa kwa walimu imeelezwa kwenye kanuni Na 126 (1 hadi 3) ya kanuni za mtumishi wa umma,2003.
Muda wa kuwasilisha rufaa ni siku 45 tangu tarehe aliyopata uamuzi wa awali na rufaa ni lazima iwe kwa maandishi na inayowekwa wazi sababu za kupinga uamuzi na adhabu.Mrufani anapaswa kuipatia mamlaka yake ya nidhamu nakala ya rufaa.Iwapo hakufanya hivyo mamlaka
ya nidhamu inapaswa kuwasilisha taarifa ya mwenendo wa hatua za nidhamu na maelezo/utetezi wake dhidi ya sababu za rufaa ndani ya siku 14, nakala kwa Mrufani (kanuni 61).
*KUAJIRIWA UPYA KATIKA UTUMISHI WA UMMA*
Walimu wanaruhusiwa kuajiriwa upya katika utumishi wa umma baada ya kutumikia adhabu
kwa muda usiopungua miezi 12.Kanuni Na.120(d) ya kanuni za utumishi wa Umma 2003 imeelekeza kuwa kamati ya mkoa inatoa uamuzi juu ya suala hilo. Uamuzi wa kamati ya mkoa utawasilishawa kwa katibu wa tume kwa ajili ya kuwaombea kibali cha kuajiriwa upya walimu hao kwa katibu Mkuu kiongozi.
*HITIMISHO*
Lengo la mada hizi ni kuwaelimisha na kuwajengea uwezo Waratibu Elimu Kata (MEK's) ,Walimu
wakuu wa shule /Wakuu wa shule na Walimu wote kwa ujumla katika kutekeleza majukumu mbalimbali katika maeneo yenu ya kazi kwa kuzingatia sheria ,kanuni,taratibu na miongozo mbalimbali inayotolewa na serikali katika kuboresha Utumishi wa umma, mara kwa mara.
*POSHO YA KUJIKIMU*
Kanuni ya 13 inaeleza kwamba Mtumishi wa Umma aliyeajiliwa anastahili kupewa:-
Nauli yeye na mkewe/mumewe,watoto na
wategemezi wasiozidi 4. Posho ya kujikimu kwa kiwango na idadi ya siku itakapokuwa imeandaliwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais menejiment ya Utumishi wa Umma.
*KUTHIBITISHWA KAZINI.*
Kanuni Na.14 za 2003,Mtumishi wa Umma aliyeajiliwa kwa masharti ya kudumu atakuwa chini ya matazamio kwa kuzingatia muundo wa Utumishi wake na haitazidi miezi kumi na
miwili.
Mkuu wa kituo/kazi atawajibika kutoa taarifa kwa mamlaka husika kuhusu:-
Mtumishi kuthibitishwa kazini.
Mtumishi kuongezewa muda wa matazamio ili kumwezesha kufanya kazi kwa ufanisi.
Utumishi wa Mtumishi kusitishwa.
*KUPANDISHWA CHEO (KANUNI NA.15)*
Kupandishwa cheo kwa Mtumishi wa Umma kutategemea muda wa uutendaji,utendaji wa kazi uliokidhi malengo (ufanisi wa kazi) na Taaluma ya Mtumishi.
Mtumishi akipandishwa cheo atakuwa kwenye matazamio kwa muda wa miezi 6.Kanuni Na.16(1).
*UHAMISHO.*
Mtumishi anapohamishwa hustahili mambo yafuatayo;-
Posho ya usumbufu asilimia 10 ya mshahara wa mwaka (Kanuni za kudumu za 2009 L(3: 1- 2).
Posho ya kujikimu atalipwa atalipwa siku 14 akiwa na mweza wake na watoto wake 4 chini ya umri wa miaka 18 na wategemezi 2 kanuni za kudumu 2009 L(1-2).
Usafiri wake na familia yake pamoja na mizigo isiyo chini ya Tani tatu kutegemea na daraja
lake 9 kanuni za kudumu za 2010 J1).
*UHAMISHO WA KUOMBA.*
Mtumishi wa umma hatalipwa chochote anapoomba uhamisho kwa manufaa yake (isipokuwa)kama amekaa kituo kimoja sio chini ya miaka mitano mfululizo au kama anataka kwenda kwao
kujianda na kustaafu na awe amefanya kazi nje ya mkoa wake si chini ya miaka 10 mfululizo.(L.8 a-b)
*KUSTAAFU.*
1.Kustaafu kwa hiari.
Itakuwa miaka hamsini na mitano.
Sharti atoe taarifa ya kusudio lake miezi sita kabla ya kutimiza miaka 55.
2.Kustaafu kwa ugonjwa.
Kanuni namba 30,2003
Sheria namba 2 ya pensheni ya itimisho la kazi.
Kwa ushauri wa daktari au jopo la madaktari mamlaka inaweza kupendekeza mwalimu astaafu
kwa ugonjwa.
3.Kustaafu kwa lazima.
Mtumishi wa umma atalazimika kustaafu kwa lazima atimizapo umri wa miaka sitini.
Atawajibika kutoa taarifa miezi sita kabla ili aweze kupata kibali kwa wakati .
*MAFAO YA KUSTAAFU.*
PENSHENI/MIRATHI/KIINUA MGONGO cha mkataba wa muda
maalum.
*PENSHENI.*
Pensheni ni mafao ya hitimisho la kazi kwa mtumishi anaye staafu kwa:-
lazima: Miaka 60.
kwa hiari: Miaka 55.
kwa ugonjwa
Pensheni inayolipwa na hazina ni kabla ya 1.7.2004, hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 73 (2) cha sheria ya mafao ya hitimisho la kazi na 2 ya 1999.
*NIDHAMU,AINA ZA MAKOSA NA ADHABU ZAKE.*
Sera ya menejimenti na ajira katika utumishi wa umma ya mwaka 1999 katika aya za 5.37-37
zimeeleza kuwa KOSA ni kitendo cha utovu wa nidhamu kutokana na kukiuka maadili, kanuni
na masharti ya kazi.
Utaratibu wa kuzingatiwa katika kushughulikia utovu wa nidhamu umeelezwa bayana na kwamba adhabu zitatolewa kulingana na uzito wa kosa.
Kwa mujibu wa kanuni Na.42 (2) na 43 (2) za kanuni za utumishi wa Umma za mwaka 2003,aina za makosa na adhabu zake zimeainishwa katika nyongeza Na.2.
*MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKUA HATUA ZA NIDHAMU.*
(A). Uchunguzi wa awali. Kanuni Na.36 ni lazima mamlaka ya nidhamu ifanye uchunguzi wa awali kabla haijaanza hatua za nidhamu dhidi ya mtumishi. Hatua hii inasaidia kugundua
ukweli kuhusu ukiukwaji na kujiridhisha kuwa mtumishi amehusika na kuwa kuna
uwezekano wa kuthibitisha kosa dhidi yake.
Hatua hii inapunguza uonevu unaoweza kuwepo kwa uchukuaji wa hatua za nidhamu kwa pupa.
(B). Makosa na adhabu,kanuni Na.53 na 59.
makosa madogo madogo (summary
proceedings) kanuni Na. 43.
-kuchelewa kufika kazini
-kutokuwepo kazini muda wa kazi
-kutokamilisha kazi.
-uzembe katika kutekeleza majukumu.
-kutotimiza maelekezo ya utendaji kazi.
Mara ya kwanza – barua ya onyo
Mara ya pili – karipio
A ya tatu – kusimamisha nyongeza ya mshahara.
(C).Makosa makubwa (formal proceedings) kanuni Na.42
-kutofika kazini zaidi ya siku 5
-vitendo vinavyohusu wizi,rushwa
-uzembe uliokithiri katika kutekeleza majukumu.
-kujihusisha na kazi nyingine nje ya ofisi saa za kazi.
*VITU VYA KUANDAA UNAPOJAZA*:
*1.MKATABA WA AJIRA*
FOMU ZA MKATABA NAKALA 3
PICHA ZA UTUMISHI
CHETI CHA TAALUMA (UALIMU NAKALA 3
CHETI CHA FORM FOUR/SIX NAKALA 3
*2.USAJILI WA PENSHENI*
1.BARUA YA AJIRA (YENYE TSD NAMBA)
2.BARUA YA KUTHIBITISHWA KAZINI
3.SALARY SLIP HALISI
4.PICHA 2
*3.KUSTAAFU*
1. BARUA YA AJIRA (YENYE TSD NO)
2. BARUA YA KUTHIBITISHWA KAZINI
3. BARUA YA KUPANDA CHEO CHA MWISHO
4. SALARY SLIP
5. PICHA TATU
6. KIBALI CHA KUSTAAFU (ukipate TSD Wilaya)
7. UJAZE FOMU ZA PSPF NO 6.
*4.KUANDAA MIRATHI MAHITAJI*
1.MUHTASARI WA WANANDUGU
KUMCHAGUA MSIMAMIZI WA MIRATHI
2.HATI YA USIMAMIZI WA MIRATHI (HALISI)
3.CHETI CHA KIFO(HALISI)
4.BARUA YA AJIRA(YENYE TSD)
NAKALA
5.BARUA YA KUTHIBITISHWA KAZINI (NAKALA)
6.BARUA YA KUPANDA CHEO CHA MWISHO (NAKALA)
7.SALARY SLIP-(HALISI)
8.CHETI CHA NDOA/ KIAPO CHA NDOA (NAKALA)
9.KIAPO CHA MJANE/MGANE KUTUNZA WATOTO
10.VYETI VYA KUZALIWA WATOTO/ KIAPO(CHINI MIAKA 21)
11.BARUA TOKA SHULENI
KUTHIBITISHA KAMA MTOTO
ANASOMA
12.PICHA 8 ZA MSIMAMIZI WA MIRATHI
13. PICHA 3 ZA KILA MTOTO WA
MAREHEMU
14. PICHA 3 ZA MJANE/MGANE
15.KADI ZA BENKI ZA WALIOPO
KWENYE MGAO(NAKALA)
16.FOMU NA VI YA MGAWO WA
MIRATHI(Ofisini utapewa)
17.FOMU NA8 NA 9 ZA PSPF (Ofisini utapewa)
VYOTE LAZIMA VIPITIE MAHAKAMANI NA MHURI NA SAINI YA HAKIMU.
KILA MTU AVIANDAE AU ATUNZE KUMBUKUMBU ZA UTUMISHI KWA SABABU NI
TUKIO LA KILA MTU.
*IMETOLEWA NA TUME YA UTUMISHI WA UMMA IDARA YA UTUMISHI WA WALIMU.
aPosted via Blogaway